WASOMI HURU GEREZANI.
January 6, 2021 at 2:46 pm,
No comments
Kuna wakati huwa najiuliza maswali ambayo mengine huwa yananifanya niwashangae sana wasomi.
Ikiwa mtu fulani anasema na hata kujiita kwamba yeye eti ni msomi na ni kweli kabisa kwamba yeye ni msomi lakini mtu huyo huyo anaejiita kuwa ni msomi utakuta analalamika mno kwamba na yeye hana ajira, analalamika kweli huku akisema kwamba anasubiri ajira zitoke ili ndiyo maisha yaweze kwenda.
Swali langu huwa ni hili, Sasa ndiyo msomi gani huyo ambaye anashindwa kutatua hata changamoto yake tu ya kupata ajira?
Ina maana kwa usomi wake kweli kakosa kitu cha maana cha kufanya ambacho kinaweza kikawa bora kufanya maisha yake yasonge?
Hapa sasa ndiyo huwa namkumbuka baba wa falsafa Socrates. Kuna siku Socrates aliwasha taa mchana kweupe kabisa na kwenda nayo sokoni huko ugiriki. Watu walimshangaa sana, wengine walimcheka tu kabisa, lakini wachache wenye akili walimuuliza kwa nini anafanya vile wakati ni mchana? Alichowajibu Socrates ni kwamba, pamoja na nuru ya jua iliyopo bado akili za watu wengi zilikuwa kwenye giza zito, hivyo alikwenda kuzimulika ili waweze kuzitumia akili zao kutafuta majibu sahihi ya changamoto zinazowakabili.
Kitabu hiki cha Denis Mpagaze kimewashwa mchana kweupe kama taa ya Socrates kutumulikia sisi wasomi kuzitumia akili zetu vizuri ili tuweze kupata majibu ya changamoto zinazotukabili.
Muhimu kwako kufanya hivi sasa ni kuamua tu kusoma kitabu hiki.
Kitabu kinapatikana CITYMAX BOOKSHOP.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu 0753690907 au 0754086824
CITYMAX BOOKSHOP.
Tunaboresha Maisha Yako.
Tembelea website yetu (http://www.citymaxbookshop.mozello.com );
Facebook page yetu na Instagram account yetu kwa maelezo zaidi.
Kujiunga na kundi letu la wasapu la CHUO CHA MAARIFA ili uweze kujifunza zaidi, tutumie ujumbe wasapu kwa namba 0672134512
Kupata Huduma Zetu Za Ukocha, Wasiliana Nasi Kwa Namba 0672134512 au 0753690907
KARIBU SANA CITYMAX BOOKSHOP.